Beki wa
zamani wa Barcelona na Uhispania Carles Puyol amepigwa marufuku kushiriki
kipindi cha kombe la dunia nchini Iran kwa kuwa na nywele ndefu.
Licha ya kukubali kushiriki
kwenye kipindi cha kutangaza mechi ya kombe la dunia kati ya Uhispania na Iran,
na hata kuwasili Iran, Puyol alilazimika kusalia kwenye hoteli baada ya
kunyimwa ruhusa kutangaza mchuano huo.
Puyol alitarajiwa kushirki
kipindi hicho spesheli kwenye kituo cha IRTV 3 akiwa na mtangazaji Adel
Ferdosipour.
"Namna mnavyojua, nilitarajiwa kuwa na Carles Puyol
studioni leo, lakini yuko hotelini kwa sasa. Licha ya juhudi zangu zote,
hatukufanikiwa. Tunaomba radhi,"Ferdosipour
alisema.
Bwana Puyol alifahamishwa na
idhaa ya taifa ya IRIB hangeweza kushiriki kwenye kipindi kwani nywele zake
zilikuwa ndefu.
Idhaa ya taifa ya Iran haina
sheria juu ya mtindo wa nywele lakini mambo yanayokinzana na mafunzo ya
Kiislamu huzuiwa.
Aidha, sheria za shirikisho la
soka la Iran zinawazuia
wachezaji dhidi ya kuwa na mtindo
wa nywele
'unaoeneza
mitindo ya kigeni' na wachezaji
huonywa dhidi ya kuwa
na
mitindo ya nywele inayokatazwa.
Hii sio mara ya kwanza hali kama
hii kushuhudiwa kwenye runinga ya Iran.
Miaka miwili iliyopita, kipa wa
timu ya taifa ya soka ya ufuo Peyman Hosseini, alizuiwa kushiriki kipindi cha
televisheni kwa sababu ya nywele zake. Aidha, alikataa pia kuzifunika.
Uamuzi wa kumzuia Puyol unajiri
wiki chache tu baada ya mkurugenzi wa IRTV3's Ali Asghar Pourmohammadi,
kuondolewa na nafasi yake kupewa afisa mwenye misimamo mikali ya kidini.
Hata hivyo naibu mkuu wa idhaa ya
taifa (IRIB), Morteza Mirbaqeri amenukuliwa Jumamosi akipinga madai hayo.
Shirika la Jam-e Jam daily linalomilikiwa na IRIB,
limemtaja bwana Mirbaqeri akisema "Idhaa ya taifa inapinga madai hayo
asilimia 100% ".
0 Comments