Mkuu wa wilaya ya Singida Elias Tarimo |
MKUU wa Mkoa wa Singida,Dk.Rehema Nchimbi amewaagiza viongozi wa
vyama vya ushirika kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo ya ushirika kuanzisha
viwanda vya kuongeza thamani ya mazao katika vyama vyao vya ushirika.
Dk.Nchimbi ametoa agizo hilo katika hotuba yake ya ufunguzi
iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Singida,Bwana Eliasi Tarimo
kwenye uzinduzi wa jukwaa la wanaushirika Mkoa wa Singida lililofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki mjini Singida.
Aidha mkuu wa wilaya huyo hata hivyo ameweka bayana kwamba mkoa
wa Singida ni maarufu kwa uzalishaji wa mazao mchanganyiko ikiwa ni pamoja na
alzeti,mtama,pamba,mazao ya mifugo,lakini hakuna viwanda vya ushirika
vilivyoanzishwa kwa ajili ya kusindika mazao hayo.
Kwa mujibu wa Mkuu huyo wa Mkoa ni wajibu wa viongozi na
wanachama wenyewe kuhakikisha vyama vinatunza mitaji yao ya ndani kwa kuweka
akiba mara kwa mara,kulipa hisa,kuweka amana naa kutenga mafungu ya lazima
kutokana na faida na kutafuta vyanzo vingine vya fedha.
Akisoma taarifa ya Maendeleo ya ushirika ya Mkoa wa Singida kwa
niaba ya Mrajisi msaidizi wa Mkoa,Afisa ushirika wa Halmashauri ya Itigi,Bwana
Charles Martin Madula amefafanua kwamba ni ukweli kwamba ushirika wa mazao
mchanganyiko yakiwemo mazao ya alzeti,ufuta,dengu,mbaazi na pamba umekuwa
haufanyikazi ya kuwahudumia wanachama wake kwa kipindi cha kirefu sasa.
Kwa upande wake Mwakilishi wa vyama vinavyplima zao la tumbaku
katika Halmashauri ya Itigi,Wilayani Manyoni,Bwana Martin Petro Mdemwa ameweka
bayana kwamba vyama vya Idodomya Amcos,Manyanya Amcos,Isingiwe Amcos,Mtakuja
Amcos na Umoja Amcos vinakabiliwa na changamoto ya soko la kuuzia kilo
58,770.14 za tumbaku.
Mwana ushirika wa ufugaji Nyuki na mshindi wa nane nane mwaka 2017 Bw Kiemi akitoa ushuuda wake katika ulinaji wa asali. |
mwanaushirika kutoka katika sekta ya madini akitoa ushuhuda wake pia. |
Baadhi ya wanaushirika mkoa wa Singida wakipiga picha na mgeni rasimi. |
0 Comments