Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Singida ACP Debora Magiligimba akionyesha mihadarati hiyo ofisini kwake.
|
Kamada Mgailigimba akiwa katika ukaguzi wa magari barabara kuu ya Mwanza. |
Mbwa wa Polisi akikagua basi la Mgamba kutoka Arusha kwenda Mwanza. |
Jumla ya misokoto 7360 ya
bangi imekamatwa na jeshi la polis mkoa wa Singida pamojana na kilo 41 na gramu
220 za milungi katika operesheni inayoendelea nchi nzima ya kupambana na madawa
ya kulevya.
Akitoa taarifa kwa vyombo
vya habari kamanda wa jeshi la polis mkoania Singida ACP Debora Magiligimba
amesema oparesheni hiyo imeanza tarahe 1mwezi wa pili mwaka huu na kufanikiwa
kukamata madawa ya kulevya ya aina mbalimbali
Kamanda Magiligimba amesema
wanafanya ukaguzi wa mabasi yanayoingia mkoani hapa kwa kutumia mbwa ambao
wamaepata mafunzo ya kubaini madawa hayo
Amesema watuhumiwa saba
wamefikishwa mahakamani kwa kujihusisha na biashara hiyo huku watuhumiwa
13,wakisubiri majarada yao kukamilika kwa hati za mashtaka kutoka kwa
mwanasheria wa kanda mkoa wa Singida.
Amesema zoezi hilo ni
endelevu huku akiwaomba wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha
wanatokomeza la madawa ya kulevya
0 Comments