DC IKUNGI AGEUKA MBOGO JUU YA MIGOGORO YA ARIDHI.

MKUU wa wilaya Ikungi Mkoa wa Singida Thomas Apson amewataka watu wanoendesha au kuibua mogogoro ya aridhi vijijini wanaache tabia hio mara moja ili kuepusha hasara na upotovu wa muda na maendeleo kwa wananchi kwa kuacha kufanya shughuli za kujiletea mapato kwa jamii.

Dc Thomas alidokeza kuwa mahali popote penye migogoro na vipingamizi vya matumizi halali ya ardhi hakuna maendeleo watu wanashindwa kufanya kazi za kujiongezea mapato wanahangaika kila siku kesi mahakama mwishowe mpaka rufaa Dodoma hii ni nini taba gani hii katika jamii kwa Ikungi tabia hii iwe mwisho.


Kumekuwa na watu wenye tabia za kuanzisha kesi hizo vijijini hasa nyakati za masika na wengine huibua migogoro ya uvushaji wa mipaka halali iliowekwa ili apambane mahakamani Ikungi hatutaki watu wa jinsi hiyo.

“ Tokeni kwenye jamii ya mfike kwenye jamii ya maendeleo migogoro ya kuunda iacheni, migogoro ya kuibua iacheni itatupotezea muda mwingi wa kufanya kazi za maendeleo ya taifa”. Alisisitiza DC.

Mkuu wa wilaya ya Ikungi Thomas Apson aliyesema hayo juzi katika moja ya ziara zake wilayani Ikungi alipotembelea wanachi wa tarafa ya Sepuka na kusikiliza kero zao wakiongozana na Mkurungezi wake Lawrence Kijazi.

Mkuu huyo wa wilaya amewataka wananchi wa tarafa ya sepuka kuacha kuenesha na kuibua migogoro ya ardhi ili kuepusha usumbufu katika jamii akawaagiza maafisa ardhi kuenda kusimamia ardhi zenye kesi na kuzipatia ufumbuzi na kama uwezekano upo ardhi ipimwe upya.

c Ikungi amewaomba wananchi wa wlaya ya Ikungi kuisi kwa amani na utulivu ili wapate muda mwingi wa kufanya kazi za maendeleo amewataka wanachi kuchukua muda mwingi kufanya kazi za kujiongezea kipato waachane na uibuaji wa migogoro ya ardhi katika jamii


=MWISHO=

Tuandikie Maoni Yako Hapa

Post a Comment

0 Comments