VIONGOZI wa Dini hapa nchini wameaswa kutafuta sana amani kwani ndio moja ya silaha katika kuyafikia maendeleo na kwamba wao ndio wenye nguvu ya kuhamasisha jamii kuitafuta hiyo amani.
Mwenyekiti wa kitaifa wa shirikisho la familia kwa amani ya Dunia (FFWP) na shirikisho la Dini mbalimbali la amani na maendeleo (IAPD) hapa nchini Stylos Simba mwene alitoa wito huo jana wakati alipokuwa mgeni rasmi katika kongamano la Viongozi wa Dini mbalimbali Mkoa wa Singida.
Kiongonzi huyo alisema Viongozi wa Dini wanakazi kubwa ya kuhakikisha hawachoki katika kuwaelimisha,kuwahamasisha watu kwenye nyumba zao za ibada ili kwa pamoja amani iendelee kuwepo na hatimaye taifa liwe na maendeleo makubwa.
"Amani inaanzia kwa mtu binafsi, familia na taifa.Na amani ni chanzo cha maendeleo,Kwa mtu,familia na hatimaye taifa..tuitafute amani." alisema Simbamwene.
Alisema lengo la kongamano hilo lililowakusanya Viongozi wa dini mbalimbali,washiriki wengine wa shirikisho hilo zaidi ya 600 mkoani hapa ni kukumbushana suala la amani na kwamba dini zisiwafarakanishe watu bali zitumike kama njia za kumrudia Mungu.
"Sisi asili yetu ni moja tumetoka kwa baba moja haina haja ya kugombana,dini ni njia tu..tusibanguane." alisema Simbamwene.
Awali akisoma risala kwa niaba ya shirikisho hilo mkoa Juma seph ambaye pia ni katibu msaidizi wa shirikisho hilo Wilaya ya Iramba alisema mkoa umefanikiwa kuwa na wanachama zaidi ya 1,700 waliojiunga na shirikisho hilo.
Pamoja na wanachama hao shirikisho hilo mkoa limetenga eneo lisilopungua ekari 500 kwa ajili ya kuanzisha ufugaji wa nyuki kama ilivyo kauli mbiu yao ya upendo,umoja,amani na maendeleo kwa dini mbalimbali.
Aidha Mwenyekiti wa shirikisho hilo Mkoa wa Singida Askofu Wilson Mtatuu alitumia fursa hiyo kuupongeza uongozi wa kitaifa wa shirikisho kukubali na kuona kuwa kuna haja ya makao makuu ya shirikisho hilo kuwa Singida.
"Hii ni fursa kwetu wanasingida tulitumie shirikisho hili ili tupate maendeleo,naamini tukiwa na amani tutafanya kazi na hatimaye tutapata maendeleo." alisema Askofu Mtatuu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa mawasiliano wa shirikisho hilo taifa Bishop Dkt Doulos Gamba alisema Viongozi wa Dini wameacha kufundisha biblia ama Quran badala yake wamekuwa wakihangaika na Dini ya mtu hayo mambo yamepelekea kuhatarisha amani
Aliwaomba viongozi hao kutotengana na badala yake wafanye kazi kwa pamoja kwasababu wote wametoka katika asili moja Dini zisiwagawanishe.
Viongozi wa Dini mbalimbali Mkoa wa Singida wakiombea maji waliyoyamimina kwa
pamoja kwenye chombo kilichopo mbele yao kama ishara ya ushirikiano.
Askofu Jonas Kaaya kutoka kanisa la Pentekoste Singida akizungumza jambo kwenye kongamano la Viongozi wa Dini mbalimbali Mkoa wa Singida.
Mkurugenzi wa mikusanyiko hapa nchini kutoka shirikisho hilo Bishop Dkt
Machimbya akitoa neno katika kongamano hilo.
Mwenyekiti wa kitaifa wa shirikisho la familia kwa amani ya Dunia FFWP na shirikisho la Dini mbalimbali la amani na maendeleo IAPD, Stylos Simba mwene Akizungumza kwenye kongamano hilo alipokuwa mgeni rasmi.
Wanakongamano wakifuatilia matukio mbalimbali.
0 Comments