Mkurugenzi wa asasi inayojihusisa na uoteshaji miti mkoa wa Singida ADESE Bw Kitanto Ramadhan Saidi wakati akiongea na mwandishi wetu ofisini kwake.
Katika kuhakikisha swala la mabadiliko ya tabia nchi yanaendelea kufanyiwa kazi ili kuepukana na majanga mabalimbali yanayojitokeza sasa ya ukatwaji wa miti hovyo ,wingi wa mifugo bila mpangilio na kusababisha ukame na upungufu wa mvua.
Asasi ya Lungo tiba asili kwa kushirikiana na asasi mbalimbali na serikali ya mkoa wa Singida imepanga mpago wa upandaji wa miti dawa katika kila kata zote za mkoa wa singida.
Katibu wa Asasi hiyo ya Lungo Tiba asili Bw.Musa Mazoya Musa akiongea na waandishi wa habari katika kitalo cha miche ya miti hiyo kilichopo katika ofisi ya mkuu wa wilaya ya Singida amesema kuwa lengo la upandwaji wa miti hiyo ni kurudisha uoto wa miti tiba iliyokuwa ikutumika kwa tiba enzi za zama za kale.
Nea mkurugezi wa kikundi cha hiyari kinacho jiusisha na kuhifhadi na kuboresha mazingira mkoa wa Singida(ADESE) Bw Kitanto Ramadhani Saidi amesema kuwa wamefanikiwa kuotesha aina mbalimbali ya miti dawa kwa kushirikiana na wataalamu wa tiba asili.
0 Comments