Chama
cha mapinduzi Kata ya Mikocheni kimefanya zoezi la utekelezaji wa ilani kwa
kutembelea miradi inayotekelezwa katika kata hiyo.
Ziara
hiyo imeongozwa na Diwani wa Kata hiyo Eng Zenzely Hussen Iddy akiambatana na
watendaji wa Kata,Mitaa na Viongozi wa Kamati Mbalimbali wa Chama cha
Mapinduzi.
Diwani
wa Kata ya Mikocheni Eng Nzenzely Hussein katikaki wakiwa kwenye ukaguzi wa
miradi ndani ya Kata ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama.
Hamisi
Malela Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amezungumza kwaniaba ya Wanafunzi na Walimu
wa shule amesema kujengwa kwa maabara kutaongeza ufaulu kwasababu shule hiyo
inafanya vizuri katika masomo ya sayansi wakiwa hawana maabara wanatumia
madarasa.
Pia
Eng Angel Michese msimamizi wa mradi huo amesema ujenzi unaendelea vizuri mpaka
kufikia mwezi wa kwanza mradi utakuwa umekamilika.
Mradi
wa vyumba vya madarasa ya Ghorofa na Maabara tatu (3) Kemia, Fizikia na Baiolojia
shule ya sekondari Mikocheni.
Sanjari
na mradi huo pia wambelea mradi wa barabara ya Regent ambao umekamilika kwa
kiwango cha lami na kugharimu zaidi ya shilingi milioni 676 yenye urefu wa km
0.64.
Pichani
barabara ya regent iliyo kamilika kwa kiwango cha lami.
Vilevile
wametembelea barabara ya chwaku yenye urefu wa km 0.6 kwa kiwango cha lami
utekelezaji unaendelea kukamilisha mradi huo.
Pichani
barabara ya Chwaku ikiwa katika matengenezo.
Aidha
walitembelea mradi wa kisima cha maji ulipo Mikocheni À ambao unajumisha jumla
ya visima kumi na sita vilivyo jengwa katika kata hiyo ambavyo vimepunguza
hadha ya upatikanaji wa maji ambao ulikuwa changamoto kwenye kata hiyo.
Mradi
wa kisima cha maji uliopo mikocheni mtaa wa darajani kilichofaziliwa na
YilmazMehmet Ali Dertop.
0 Comments