Uganda imejizolea pointi nne katika kundi E kwenye mechi za
kufuzu kwa kombe la dunia kwa kuwatandika Congo Brazzaville bao 1- 0.
Bao hilo lililofungwa na mshambuliaji Farouk Miya mnamo dakika
ya 18 liliwaweka Crane Uongozini na kuwapandisha katika jedwali hadi namba moja
katika kundi lao.
Miya ambaye huijizea Standard Liege nchini Ubelgiji alidhibiti
mpira na kuvurumisha kombora kali lililomchanganya kipa wa Congo Brazzavile
Mongondza Ngobo.
Kwngineko Afrika kusini iliwashinda Senegal kwa mabao 2-1 na
kuingia kilele mwa kundi D.
Hii nido mara ya kwanza Senegal inashindwa tangu ipoteze kwa
Algeria wakati wa mechi za makundi kuwania kombe la taifa bingwa barani Afrika
mwaka 2015.
0 Comments