
Trump amesema uamuzi huo utategemea utawala wa kikomyunisti
mjini Havana, kuweka sera ambazo zitaimarisha hali ya maisha kwa raia wa nchi
hiyo, na wale waliochukua uraia wa Marekani na wale wa Marekani.
Utawala wa rais Obama umejitahidi kurejesha uhusiano na utawala
wa Havana, baada ya uhasama uliodumu kwa zaidi ya miaka hamsini.
Trump amemtaja marehemu Castro kama kiongozi mkatili wa kiimla
ambaye aliwakandamiza raia wake kwa miongo kadhaa.
0 Comments